Chama cha mpira cha Urussi
kimethibitisha habari za kua aliyewahi kua Kocha wa klabu ya Real Madrid
na England Fabio Capello ndiye Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya nchi
hiyo.
Punde baada ya kutangazwa Capello mwenye umri wa
miaka 66 amesema shabaha yake ni ufanisi wa haraka. Ledngo langu ni
kuiwezesha Urussi kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil,
alisema Capello.
Nilipomaliza kazi ya England, nilikua na
ghadhabu na nilitaka kuendelea kufanya kazi. Ukweli ni kwamba nataka
kutimiza malengo yenu Urussi na kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.
Capello alikuwa kwenye orodha ndefu iliyokuwa na
majina ya magwiji kama Harry Redknapp, ambaye chama cha mpira cha
Urussi kilimtaka awe Kocha wake mpya.
Kocha huyo aliacha sifa ya kiwango kikubwa cha
ushindi kuliko waliomtangulia England akishinda asili mia 67% ya mechi
ingawa Timu yake ilipata shida kwenye mashindano ya Kombe le Dunia
nchini Afrika ya kusini mwaka 2010 ilipoondolewa mapema na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment