Mahakama Kuu ya kikatiba nchini
Misri ambayo mwezi uliyopita ilitangaza amri ya kuvunjwa kwa bunge la
nchi hiyo inatarajiwa kujadili hatua ya Rais Muhammed Murisi ya
kutangaza bunge liendelee na shughuli zake.
Spika wa bunge hilo tayari ametangaza kuwa wabunge wakutane siku ya Jumanne kwa vikao vya bunge.
Wakuu wa jeshi na maafisa wa mahakama wamefanya vikao vya dharura lakini hadi sasa hawajatoa uamuzi wowote.
Rais Mursi, ambaye chama chake cha Muslim
Brotherhood kilishinda viti vingi amesema bunge lazima liendelee na
vikao vyake wakati uchaguzi mpya ukiandaliwa.
Lakini kufikia sasa jeshi bado limezunguka bunge
hilo na haijulikani ni lini au vipi wabunge hao watakutana na kuendelea
na vikao vyao.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo Jon Leyne anasema
kwamba itabidi wabunge hao wafanye bidii ili wauvunje ukuta wa polisi na
jeshi ambao uko nje ya majengo ya bunge kabla ya wao kufaulu kuingia
ndani au basi itawabidi wakutana kwengine.
Baraza kuu la kijeshi ambalo hivi karibuni
lilitangaza kuwa limejitwika mamlaka ya bunge lilifanyaka kikao cha
dharura muda mfupi tu baada ya Rais Mursi kutua amri ya bunge kukutana.
Baraza hilo linatarajiwa kufanya kikao chengine tena.
Jeshi lilijitwika madaraka likikidai kwamba
lilikuwa tekeleza amri ya mahakama kuu ambayo ilivunja bunge kufuatia
malalamiko kuhusu viti vilivyotengewa wagombea huru.
No comments:
Post a Comment