KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
Baadhi ya madaktari waliokwenye
mafunzo ya vitendo katika hospitali ya taifa Muhimbili wameanza
kuondoka kurudi makwao baada ya serikali kuwaamrisha kufanya hivyo kama
hawaridhishwi na kiwango cha malipo ya posho wanazopewa.
Wakati Madaktari hao wakiondoka
tayari serikali kupitia Wizara ya Afya na ustawi wa jamii imewataka
ambao wamepewa barua kuripoti kwa katibu mkuu wa wizara ifikapo july 6
mwaka huu kutokana na kujiingiza kwenye mgomo.
Kuondoka kwa madaktari hao
kunadaiwa kuzidisha pengo la utoaji huduma kulikotajwa juzi na
mwakilishi wa Madaktari bingwa hospitali ya Taifa Muhimbili Catherine
Mng’ong’o wakati akitoa tamko la madaktari bingwa kwamba hawapo tayari
kufanya kazi bila madaktari wasaidizi.
Uchunguzi uliofanywa na Clouds Fm umegundua kwamba baadhi ya wagonjwa wameanza kurejea
kwenye hospitali ya Muhimbili kupatiwa huduma za matibabu baada ya
baadhi ya madaktari kuanza kurejea kazini wakiwemo madaktari wa watoto
pamoja na tiba nyingine.
No comments:
Post a Comment