SALMA Jabu ‘Nisha’, aliye msanii wa filamu Bongo, ameendelea kujinadi kutoka na jamaa anayedaiwa ni mume wa mtu aitwaye Geofrey Kusila ambapo safari hii amemuandalia bonge la ‘bethidei’, Risasi Mchanganyiko limechungulia.
Tukio hilo ambalo Nisha ameonekana kulifanya bila hofu wala kificho lilidakwa na paparazi wetu Jumapili iliyopita katika Baa ya Uhuru Peak, Mwananyamala jijini Dar ambapo wasanii kibao walihudhuria.
Awali, chanzo kilichokuwepo eneo la tukio kilimuendea hewani paparazi wetu na kumtonya kuwa Nisha amemfanyia ‘surprise’ jamaa huyo kwa kumuandalia pati ya kimyakimya ndipo akatinga eneo hilo na kujionea kila kitu.
ENEO LA TUKIO
Paparazi wetu alifika eneo la tukio na kushuhudia shamrashamra za kulishana keki zikiendelea kabla hajawapiga picha za kumwaga lakini baadaye mtiti ukaibuka na kuamriwa azifute.
“Jamani hebu acha kupiga picha na unatakiwa kufuta zote ulizopiga. Yaani nyie hampitwi! Kwanza nani amekualika hapa?” alihoji Nisha kwa hasira.
Hata hivyo, mwandishi wetu alifanikiwa kuwachomoka bila kufuta picha hizo.
Aidha, juzi Jumatatu gazeti hili liliwasiliana na Nisha kwa njia ya simu na kumwuliza juu ya sakala hilo, akasema: “Ni mchumba’ngu na amenivisha pete, kama angekuwa mume wa mtu angeweza kukaa nyumbani kwangu kwa muda wote huo? Ninachojua ni mpenzi wangu basi, sitaki maswali zaidi lakini nakusisitiza ufute zile picha.”
SASA TUJIKUMBUSHE
Miezi michache iliyopita Nisha na Geofrey walibambwa na paparazi wetu maeneo ya Mikocheni, Dar wakijiachia kimahaba na habari hiyo kutokezea gazetini.
Stori hiyo ilipotoka gazetini uliibuka mtafaruku mkubwa baada ya mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mke halali wa Geofrey kupiga simu na kuchimba mkwara mzito akidai kuwa atadili na Nisha.
No comments:
Post a Comment