Tuesday Kihangala ‘Chuz’
BOSI wa Kampuni ya Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ anadaiwa kusakwa na jamaa mmoja (jina tunalo) kwa madai ya kumtapeli kiasi cha shilingi 5,000,000 ambazo zilikuwa za makubaliano ya ufunguzi wa kampuni ya kusambazia filamu Dar ambayo haipo.
Kwa mujibu wa chanzo, jamaa huyo ambaye ni mfanyabiashara alimkopesha Chuz fedha hizo Februari 23, mwaka huu kwa ahadi ya kuzirejesha Juni 15, 2012 lakini mpaka Julai hii jamaa hajapata chake.
“Chuz alikopa fedha hizo mwezi wa pili mwaka huu, kwenye mkataba akatakiwa awe amezilipa mwezi wa sita katikati, lakini mpaka sasa hajamlipa jamaa na akimpigia simu anakata, ndiyo jamaa kaamua kumtafuta kivyake kabla ya kwenda polisi,” kilisema chanzo.
Kiliendelea kudai kuwa, mbaya zaidi jamaa ameshatia timu mara kadhaa kwenye ofisi ya Chuz, Kinondoni, lakini anakumbana na mademu wanaomwambia bosi wao amekwenda ‘lokesheni’ kumalizia ‘shutingi’ ya filamu ya Dirty Game.
“Sasa jamaa ameshatangaza kuipiga marufuku filamu hiyo isiingie sokoni kabla hajalipwa fedha zake na alisema atawatumia wanasheria wake,” chanzo kiliongeza.
Chuz alipotafutwa kwa njia ya simu, alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kumfahamu jamaa huyo.
“Namfahamu vizuri …(akamtaja jina), lakini sasa umeniuliza kama ni kweli au si kweli kuhusu mimi na yeye kukopeshana fedha, hilo siwezi kulizungumza, labda aongee yeye kama atapenda,” alisema Chuz.
Katika hali ya kushangaza, Chuz alisema habari hii ikiandikwa na kutoka kwenye gazeti atakwenda mbele ya sheria kwa sababu eti ina lengo la kumchafulia mambo yake (hakuyaweka wazi).

No comments:
Post a Comment