Meli iliyokuwa imewabeba
takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo
la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina SKAGIT ilikuwa inatoka
Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.
Jeshi
la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa
watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit
inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa
hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini
wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali
katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam
kuelekea visiwani Zanzibar.
Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa
tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya
kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Mwandishi wa BBC mjini Dar Es Salam, Aboubakar
Famau anasema kuwa meli hiyo MV Skagit ilianza kuzama saa sita saa za
afrika mashariki ikiwa inaelekea bara.
Safari kati ya bara na pwani huchukua saa mbili. Inaarifiwa huenda watoto thelathini na moja walikuwa kwenye meli hiyo.
Afisaa wa usalama katika bandari ya Zanzibar alifahamisha shirika la habari la Reuters kuwa meli hiyo sasa imebiruka.
"maiti kumi na wawili pamoja na manusura kumi tayari wameodolewa baharini kufikia sasa.
Shughuli za uokozi zinaendelea ingawa kuna
changamoto ya hali mbaya ya hewa." hii ni kwa mujibu wa waziri katika
ofisi ya rais Mwinyihaji Makame,
Kivukio kilichoko kati ya Dar es Salaam na
Zanzibar huwa na shughuli nyingi sana na huvutiwa sana na watalii pamoja
na wenyeji wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment