Kilabu moja ya soka nchini
Denmark, "Copenhagen" imekataa kumruhusu mchezaji wa kilabu hiyo Dame
Ndoye kuweza kushiriki michezo ya Olimpiki.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Senegal, alitajwa
kama mmoja wa wachezaji watatu walio na umri mkubwa kuweza kuchezea timu
ya Senegal ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 kwenye
Olimpiki.
Kulingana
na sheria za shirikisho la soka duniani, Fifa, vilabu ndio vina jukumu
la kuwapa ruhusa wachezaji walio na umri mkubwa kushiriki kwenye
Olimpiki.
Rais wa shirikisho la soka nchini Senegal,
Augustin Senghor aliambia BBC kuwa mchezaji mwingine Kalidou Yero
Coulibaly mwenye umri wa miaka 21 kutoka kilabu ya Gil Vicente nchini
Ureno atachukua nafasi ya Ndoye.
Mechi za Senegal
Tarehe 26 Julai itacheza dhidi ya Uingereza
Tarehe 29 Julai itamenyana na Uruguay.
Tarehe1 mwezi Agosti, itatoana kijasho na United Aarab Emirates.
Tarehe 29 Julai itamenyana na Uruguay.
Tarehe1 mwezi Agosti, itatoana kijasho na United Aarab Emirates.
Yero alikuwa mmoja wa wachezaji wa akiba waliokuwa wametajwa katika kikosi cha Senegal kitakachoshiriki michezo ya Olimpiki.
Senegal wataendelea na maandalizi yao ya michezo
ya Olimpiki Jumanne wiki ijayo katika mechi ya kirafiki dhidi ya
Uswizi, ambao pia walifuzu kushiriki michezo hiyo.
Kikosi cha Senegal kitakuwa kifua mbele wakati
kikijiandaa kwa mechi hiyo ya kirafiki na Uswizi hasa baada ya kushinda
Uhispania mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki siku ya Ijumaa.
Hii ina maana kuwa Senegal wana wachezaji wawili
tu walio na umriu mkubwa wala sio watatu kama inavyoruhusiwa, Mohamed
Diame, 25 anayechezea West Ham United na Papa Gueye, 28, wa kilabu ya
Metallist Kharkiv nchini Ukraine.
No comments:
Post a Comment