Mwigizaji mtoto mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jenifa Daudi ‘Jenifer’ amesema kuwa kuna baadhi ya filamu zinazotengenezwa hapa nyumbani hazistaili kuangaliwa na watoto hata kushiriki kuigiza kwa sababu zinapotosha watoto kulingana na vitu vinavyoonyeshwa katika filamu hizo, akisema kuwa filamu hizo ni za kikubwa sana.
“Sisi ni watoto wadogo ambao tunataka kujifunza mambo mazuri kutoka
kwa wakubwa kama watoto lakini kuna filamu wameshiriki watoto na ni
mbaya, Uncle Kanumba alikuwa akitengeneza filamu za watoto nzuri ambazo
zimeniletea sifa mimi na watoto wezangu na kila mtu anatupongeza kwa
filamu zile,”anasema Jenifer.
Jenifer alitolea mfano wa filamu ya House Boy ambayo imetengenezwa na
kutoka hivi karibu akisema kuwa filamu hiyo haifai kwa kutazamwa na
watoto kwani ina mambo ya ajabu sana huku ikiwa imeigizwa na mtoto
mwenzao ambaye ni Lulu, Jenifer amewasisitiza wazazi kuwa makini na
watoto katika kushiriki filamu pia kujua ni filamu zipi wanatakiwa
kuangalia.
No comments:
Post a Comment