Unakumbuka February 8 2012
wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne? stori
kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari ya bongo fleva kwenye
sehemu ya kujibia maswali.
“nashukuru sana wanaosahihisha
mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea na fani yangu ya
bongofleva, Majita wangu wako levo za juu na sio East Zuu, kukosa ni
kawaida kwa binadamu” hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7
kwenye swali la 11 kwenye moja
ya mitihani yake aliandika mistari ya bongofleva kwamba “acha utani my
girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo
ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa
mbaya”
Baada ya hayo matokeo watu
wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi, Jina lake la kuzaliwa ni
Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa sababu 5 za kwa nini
aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye mitihani yake ya
kumaliza kidato cha nne.
Amesema “1 ni kutaka kutuma
ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla, sababu ya pili ni kutaka
kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi maisha magumu kwa sababu
tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu iliyopo ambayo ukishindwa
kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna mtu anaweza akawa anashindwa
kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu kingine sasa mfumo uliopo hautoi
nafasi kwa wasioweza hiyo system, sababu ya tatu ni kutokana na
utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa sababu sijui kama kuna mwanafunzi
yeyote aliewahi kufanya mtihani wake wa mwisho alafu mtihani wake
ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na wapi alipopata”
“Sababu ya nne ni kuhusu wazazi
kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo kipi wanaweza kipi
hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni kwa serikali ijaribu
kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo kabisa, leo hii kuna
mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka mitatu na kupewa degree
ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata kimoja kwamba alikua na
elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia una degree wakati
hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea”
“Kwa namna moja au nyingine
sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu nilichofanya watu walikichukulia
tofauti sikufanikiwa ndio maana nimeamua kujitokeza kumalizia kazi
ambayo niliianza kuifanya kule kwa sababu nafsi yangu ilikua inanisuta,
ila kwa sasa watu watakua wameelewa na ninaweza kuwasaidia watu wengine”
– Julius (Elinaja)
Unaweza kulike au kutweet hii story ili na wenzako wa facebook na twitter waione, shukrani!
No comments:
Post a Comment