Rais wa FIFA Sepp Blatter
amethibitisha nia yake ya kuzidisha juhudi za kumuondoa aliyekuwa Rais
wa shirika hilo Joao Havalange kwenye uwanachama wa FIFA.
Havelange, mwenye umri wa miaka 96 pamoja na
aliyekuwa mkwe wake Ricardo Teixeira walitajwa katika hati za mahakama
hivi karibuni kuwa walipokea mlungula kutoka kwa kampuni mshirika wa
FIFA -ISL iliyofilisika katika miaka ya 1990.
Ingawa
alisema awali kuwa hakuwa na uwezo wa kuwachukulia hatua yoyote, Rais
wa sasa Blatter hivi sasa atajitahidi kuona kwamba Havalange anavuliwa
hadhi ya uwanachama wa FIFA.
Ameliambia gazeti la nchini Uswizi
SonntagsBlick: " Havelange ni milioneya wa kupindukia. Ni jambo la
kushangaza kuona kua alikubali na kupokea mlungula.Hana mahitaji ya
kutapatapa hivyo.
Nitapendekeza kwa kamati ya utendaji suala hili
lishughulikiwe kwenye kikao chetu kinachokuja. Lazima
aondolewe,haiwezekani asalie kuwa na heshima ya Rais asiye na madaraka
ya utendaji alisema Blatter.
Wababe hao wawili, Havalange na Teixeira
hawakuwahi kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu na FIFA. Badala yake
shirika hilo lilikubalia kuilipa koti faranga za uswizi milioni 2.5 kama
fidia kwa sharti kwamba kesi dhidi ya Havalange na Teixeira isiendelee
na itupwe nje ya mahakama.
Taarifa ya koti inasema kuwa Havalange kwa
uchache alipokea faranga milioni 1.5 Teixeira akapokea faranga milioni
12.74 sawa na dola za Marekani milioni 8.37 na kwa pamoja huenda
walipokea faranga milioni 21.9.
No comments:
Post a Comment