Mkutano wa kila miezi sita wa viongozi wa Umoja wa Afrika umeanza mjini Addis Ababa.
Kati ya wagombea wawili - yaani Bibi Nkosazana
Dlamini-Zuma kutoka Afrika Kusini, na mkuu wa sasa, Jean Ping, kutoka
Gabon, hakuna aliyeungwa mkono vya kutosha kwenye mkutano uliofanywa
Januari, lakini wanagombea tena.
Waandishi wa habari wanasema mashindano hayo
yamechukua muda wa mikutano, ambao ungelifaa kutazama maswala mazito,
kama mzozo wa Mali na mvutano baina ya Sudan na Sudan Kusini.
Mwandishi wa BBC anayehudhuria mkutano anasema
viongozi piya wanatarajiwa kujadili mzozo unaoendelea mashariki mwa
Jamhuri ya Denokrasi ya Congo.
Wanatarajiwa kupitisha mkakati ambao utaandaa
kuundwa wa kikosi kipya cha kimataifa, ambacho kitalinda mpaka kati ya
Rwanda na Congo na kukabili waasi ambao wanaleta fujo huko mashariki mwa
Congo.
No comments:
Post a Comment