Uhispania waingia fainali
Mabingwa watetezi Uhispania
wamefuzu kuingia fainali ya Euro 2012, baada ya kuishinda Ureno magoli
4-2, kupitia mikwaju ya penalti, baada ya muda wa kawaida wa dakika 90
na dakika 30 za ziaida kumalizika kwa timu hizo mbili kushindwa
kufungana.
Bao la mwisho la mikwaju ya penalti kwa
Uhispania lilitiwa wavuni na Cesc Fabregas, na kuwapa wenzake matumaini
ya kutetea ubingwa wao kikamilifu, watakapocheza aidha na Ujerumani au
Italia katika fainali ya Jumapili.
Fabregas,
ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Barcelona, alipiga mkwaju ambao
baada ya kugonga mwamba upande wa kushoto, ulitambaa wavuni, na ikawa ni
tiketi ya Uhispania kufanya mipango ya kusafiri hadi Kiev, Ukraine, kwa
fainali.
Mchezaji wa Ureno, Bruno Alves, alielekea kuwa
na wasiwasi, na kushindwa kufunga mkwaju wake, baada ya mpira kugonga
mwamba, na Ronaldo, akiwa amepangwa na timu yake katika nafasi ya tano
kwa wapigaji penalti, hakupata hata nafasi ya kutimiza wajibu huo.
Wengine waliokosa kufunga kupitia mikwaju ya
penalti ni mchezaji wa Ureno, Joao Moutinho, wakati kipa wa Uhispania,
Casillas, alipoweza kuokoa kwa kuruka upande wa kkulia.
Awali mchezaji wa Uhsipania Xabi Alonso naye
alikosa kutumbukiza wavuni mkwaju wa penalti, licha ya kwamba ulikuwa ni
mkwaju wa kasi na uliopigwa kwa nguvu, lakini kipa Rui Patricio
akauzuia.
No comments:
Post a Comment