Polisi Uganda wazuia basi la watoto
Suala la Ugonjwa wa kusinzia
ambao haujajulikana chanzo chake wala tiba nchiniUganda,sasa limechukua
sura mpya baada ya polisi kuzuia basi ambalo lilikuwa linawapeleka
watoto 25 mjiniKampala.
Polisi inadai kuwa walikuwa wanapelekwa huko ili
kuonyeshwa na kusema hawezi kulikubalihiloilhali mbunge mmoja alieandaa
safari hiyo akisema kuwa watoto hao walikuwa wakipelekwa hospitalini.
Serikali inasema kuwa kwa sasa watoto 3,000 ndio
wanaugua ugonjwa huo huku takriban 200 kufariki katika eneo la Acholi
tangu ujulikane mwaka wa 2009.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala Siraj Kalyango
anasema mbunge wa wanawake kutoka wilaya ya Kitgum, kaskazini mwa Uganda
,Beatrice Anywar alipanga kuwaleta baadhi ya watoto ambao wanasumbuliwa
na ugonjwa wa ajabu wa kusinzia lakini mbao si malale, katika majengo
ya bunge mjini Kampala .
Lengo la mpango wake huu anasema ni kulalamikia
jinsi serikali imejikokota kushughulikia ugonjwa huo pamoja na
kuwasaidia waathirika. Alitaka wananchi na wabunge wenzake waone hali ya
watoto hao ilivyo ya kusikitisha.
No comments:
Post a Comment