MZEE KUSEKWA: MAMA KANUMBA AACHE UJANJA
Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Mzee Charles Kusekwa.
SIKU chache baada ya habari kuwa mama wa marehemu Steven Kanumba,
Flora Mtegoa kutoka gazetini kuwa amenunua nyumba, mzazi mwenzake mzee
Charles Kusekwa ameibuka na kumtaka aache ujanjaujanja.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea Shinyanga, mzee Kusekwa alisema mama Kanumba hana fedha ya kununua hiyo nyumba ya mamilioni iliyopo Kimara - Temboni, Dar.

HII HAPA SAUTI YAKE
“Unajua mwenzangu anataka kudanganya watu, anajifanya amenunua hiyo nyumba ili iwe yake na isiingie kwenye mirathi. Anaweza kuwadanganya wasioelewa lakini mimi nasema hana pesa ya kununua nyumba.
“Aache ujanjaujanja, hiyo ni nyumba ya Kanumba na inatakiwa iingie kwenye orodha ya mirathi. Anunue nyumba kwa pesa gani aliyonayo?”

MAMA KANUMBA NAYE
Juhudi za kumpata mama Kanumba kwa njia ya simu ziligonga mwamba, lakini mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco alipopatikana alitoa ushirikiano.

TUJIUNGE NA SETH BOSCO
“Mzee anapotosha, nyumba imenunuliwa mbele ya mwanasheria na vielelezo vyote vipo. Kama ataleta kipingamizi chochote, atakutana na nyaraka zote halali.”

TUJIKUMBUSHE
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu mali za marehemu Steven Kanumba, ambapo wawili hao kila mmoja amekuwa akivutia upande wake.
Ilifikia mahali mzee Kusekwa alituma wawakilishi wake katika Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni kwa lengo la kufungua mirathi, lakini aligonga mwamba kwa kukosa hati ya kuzaliwa na kifo cha marehemu.

No comments:
Post a Comment