Mwandishi awashutumu Polisi Uganda
Mwandishi mmoja wa Uganda
amewashutumu Polisi kwa kumpiga na kumtishia kumuua baada ya kumweka
korokoroni kutokana na kitabu chake kumhusu Rais Yoweri Museveni.
Vincent Nzaramba ameiambia BBC kuwa alizuiliwa
kinyume cha sheria kwa siku tano kwa kuchapisha kitabu kinachojulikana
kama "People Power - Battle the Mighty General".
Msemaji wa Polisi alisema kuwa Bw Nzaramba alihojiwa kwa uchochezi.
nilikamatwa bila ya kuwepo hati ya kunikamata, jambo ambalo ni kinyume cha sheria, nilipigwa, niliburuzwa , waliniambia unajua tunaweza kukuua?
Mwandishi Nzaramba
Mwaka huu Uganda imekabiliwa na mfululizo wa maandamano dhidi ya utawala wa miaka 25 wa Rais Yoweri Museveni.
Nzaramba amesema Polisi walimkamata Jumamosi
baada ya kuisaka nyumba yake katika mji mkuu wa Uganda Kampala na
kutaifisha chapa za kitabu chake, komputa ya mkononi na simu.
Ushawishi wa Gandhi
Msemaji wa Polisi Judith Nabakooba alithibitisha
kuwa Nzaramba, ambaye aliachiwa huru Jumatano alihojiwa kuhusu kitabu
chake, msemaji huyo aliongeza kusema hii sio mara ya kwanza wao
kumkamata mtu kwa kumiliki nyaraka za uchochezi.
Nzaramba aliiambia BBC kuwa anashuku kama Polisi
wamesoma kitabu chake, ambacho kina picha ya Rais Museveni akiwa na
sare ya kijeshi na maandishi yanayosema "Amekwisha" yakiwa chini ya
picha hiyo.
No comments:
Post a Comment