Maporomoka yahofiwa kuuwa wengi
Shughuli za uokozi zinatarajiwa
kuanza tena leo asubuhi mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu
vilifunikwa na udongo kufuatia maporomoka ya udongo yaliyokumba eneo la
Bududa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda limesema kuwa zaidi ya watu kumi na wanane wamefariki dunia katika maporomoko hayo.
Zaidi ya nyumba kumi na tano zimezikwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.
Shirika hilo limesema maafisa wake wanaendelea
kuwatibu waliojeruhiwa katika mkasa huo, katika eneo hilo lenye rutuba
la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya
mlima Elgon.
nyumba zimefunikwa futi16 chini
Mwandishi wa habari, Stephene Mulaa, aliyezuru
eneo la tukio amesema kuwa, ''kufikia jana jioni hakuna mwili hata mmoja
ulikuwa umepatikana, kwa sababu inakadiriwa kwamba miili ya watu na
nyumba zilizofunikwa na udongo ziko zaidi ya futi kumi na sita kwenda
chini''
serikali kuwasaidia walioathirika
Serikali ya Uganda inatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusu janga hilo baadaye hivi leo.
Lakini kupitia taarifa kwa vyombo vya habari,
serikali imesema kuwa,'' inafanya juu chini kuhakikisha kuwa familia
zilizoathirika zinapata msaada wa kutosha''.
Waziri anayehusika na maswala ya majanga, Dr
Steven Malinga, amenukuliwa katika taarifa akisema kuwa hakuna madhara
makubwa yaliyoripotiwa.
Mwaka 2010, maporomoko mengine ya ardhi yalitokea katika wilaya hiyo ya Bududa, na kuwauza zaidi ya watu mia tatu.
Eneo hilo linazungukwa na miinuko pamoja na mabonde, kando kando ya mlima Elgon, na hupokea mvua kubwa katika msimu wa masika.
Serikali imewashauri wakazi katika maeneo hayo
kuhamia maeneo salama lakini wengi wamekataa kufanya hivyo wakihofia
kupoteza mashamba yao yenye rotuba.
No comments:
Post a Comment