BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Thursday, June 28, 2012

LOVENESS ANADAIWA KUYUMBISHA NDOA YA MFANYABIASHARA DAR

 Loveness Watson.
MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Loveness Watson anadaiwa kuiyumbisha ndoa ya mfanyabiashara wa magari mkazi wa Temeke jijini Dar, Peter.
Akizungumza na gazeti hili juzikati mke wa Peter, Zuwena alisema kuwa siku moja aliwakuta wawili hao wakiwa katika mkao wa mahaba ndani ya gari ambapo mumewe alishuka na kuanza kumpiga kwa madai kuwa anamfuatilia kila aendako, aliporudi nyumbani ugomvi uliendelea kisha akamtimua kurudi kwao.
Amani lilimsaka mfanyabiashara huyo na kumuwekea tuhuma zake mezani ambapo alikiri kumrejesha mkewe kwao akisema hawezi kufuatwafuatwa na mwanamke, hasa anapokuwa katika starehe zake.
Loveness ambaye pia hujulikana kama ‘Rose Ndauka Fake’, alipopatikana alikiri kuwa na mwanaume huyo lakini alidai hakujua kama ana mke.
“Ni kweli nilikuwa natoka kimahaba na Peter lakini hakuniambia kama ana mke, na mimi nikaamua kujiachia naye bila wasiwasi wowote,” alisema Loveness.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...