Sunday, April 21, 2013

Ujumbe wa mkereketwa kuhusu “Diamond” na Wema Sepetu 21/04/2013 17:49 Ujumbe uliotumwa (ambao unasomeka hapo chini) unahusiana na mazungumzo ya simu ambayo unaweza kuyasoma/sikiliza kwa kubofya hapa. WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND Kwa Kumdhalilisha Bi. Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti! Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi. Wema Sepetu, na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke." Kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kielekeza jamii kuishi kwa kufuata na kuheshimu mahadili, lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa " Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi. Penny, kitendo hiki ni cha " kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania." Tunaowaomba akinamama na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video, vcd, cd pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanya na mwamuziki. Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote wa kitanzania popote pale walipo. Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za " Udhalilishaji wa Mwanamke."

- IMEELEZWA kuwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Vanessa (jina linahifadhiwa) iliyopo Mkoani Mbeya aliyekuwa na mahusiano ya kingono mwalimu wake aitwaye John Mapunda ameambukizwa virusi vya UKIMWI (VVU). Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012 lakini hakuweza kufanya mtihani huo. Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na wakati mwingine mwanafunzi huyo alikuwa analala nyumbani kwa Mwalimu wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe. Vyanzo vya blogu ya Kalulunga vimeeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika. Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu mfululizo, wazazi walitoa taarifa Central Polisi Mbeya ambapo Polisi walianza kufuatilia. Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka kwa mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga. Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU. Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa jina la Mwashiwuya. Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika, Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe alimshitua Mwl. Mapunda na kusababisha kutorokea wilayani Chunya. Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana na tatizo hilo. Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka mambo sawa, alionekana akimfokea askari Sponsor Millinga na kwenda kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake. Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika. Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust iliyopo kata ya Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya. Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo amekuwa na kashfa ya ngono tanga akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008 baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi. Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot, mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao mkoani Tanga. Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali yeye tayari anadhani amelimaliza polisi.

11 comments:

 1. Hello colleagues, nice piece of writing and pleasant arguments commented at this place,
  I am truly enjoying by these.

  My web blog - markets.dispatch.Com

  ReplyDelete
 2. I love what you guys tend to be up too. This type of clever work and exposure!

  Keep up the awesome works guys I've added you guys to my own blogroll.

  Here is my website :: breville juice fountain

  ReplyDelete
 3. I simply could not depart your web site before suggesting that I actually
  loved the usual info an individual provide for your guests?
  Is going to be again ceaselessly in order to inspect new posts

  Here is my weblog ... kalb.It

  ReplyDelete
 4. When I originally commented I clicked the "Notify me when new comments are added" checkbox and now each time a comment is
  added I get several e-mails with the same comment.
  Is there any way you can remove me from that service? Many thanks!  Also visit my blog: omega Juicers

  ReplyDelete
 5. If some one wants expert view concerning blogging and site-building then i
  suggest him/her to go to see this webpage, Keep up the nice job.


  Look at my blog - Www.Gpva.Net

  ReplyDelete
 6. Keep on working, great job!

  Check out my website - http://178.251.198.187

  ReplyDelete
 7. I simply couldn't go away your website before suggesting that I extremely enjoyed the standard info a person provide in your visitors? Is gonna be again continuously in order to inspect new posts

  Also visit my webpage :: stil.helsingkrona.se

  ReplyDelete
 8. Hello, i think that i noticed you visited my site thus i got here to go
  back the desire?.I am trying to find things to enhance
  my site!I guess its adequate to use a few of your ideas!
  !

  Also visit my web site; “Eat Your Fruits And Vegetables”. Now

  ReplyDelete
 9. There is definately a lot to know about this subject.

  I really like all the points you've made.

  Feel free to surf to my homepage; reverse osmosis filtration

  ReplyDelete
 10. This is really interesting, You're a very skilled blogger. I have joined your rss feed and look forward to seeking more of your magnificent post. Also, I've
  shared your site in my social networks!

  my blog post: juicing recipes for juicers

  ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...