Saturday, April 13, 2013

MLELA APACHIKA DENT MIMBA

STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar. Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi. “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba. “Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho. Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo anachosoma hakijui. “Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko, kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...