Saturday, April 13, 2013

JACK WA CHUZI NAE..

KAMA kawa wiki hii katika Funguka na Risasi tunaye staa wa filamu, bibi harusi ambaye hana muda mrefu kwenye maisha ya ndoa, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’. Hapa amefungukia uhai wa ndoa yake pamoja na skendo zinazomkabili ikiwemo suala la kunaswa katika mtego wa kujiuza. Funguka: Habari za kwako Jack, vipi mzima? Jack: Mimi mzima wa afya, vipi? Funguka: Poa, nina maswali ya kukuuliza kuhusu suala zima la ndoa yako, unayaonaje maisha ya ndoa? Jack: Maisha ya ndoa ni mazuri sana na ninamshukuru Mungu kwa kunipa mume ambaye tunasikilizana na anajua nini maana ya maisha. Funguka: Nikurudishe nyuma kidogo, mume wako alilichukuliaje suala la wewe kunaswa katika mtego wa kujiuza? Jack: Mume wangu muelewa sana, anajua kazi yangu ninayofanya ya filamu hivyo vile ni vitu vya kawaida ambavyo vinaweza kutokea tu. Kipindi hicho tulikuwa marafiki tu lakini ilivyotokea ndiyo akaamua kunioa kabisa japokuwa watu walikuwa wanampa maneno mengi sana kuhusu mimi, hakuyajali hayo. Funguka: Vipi uchumba wenu ulikuwa wa muda gani? Jack: Hatukukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu, ni miezi kadhaa tu. Funguka: Kuna habari kuwa mumeo Gadner alikuwa na mwanamke mwingine na wamezaa naye mtoto mmoja na walikuwa kwenye mpango wa kufunga ndoa, hili unalizungumziaje? Jack: Ninachokijua mimi mume wangu hana mke zaidi yangu ingawa najua ana mtoto na hakuwa na mpango wa kumuoa huyo mwanamke aliyezaa naye, hayo ni maneno tu! Funguka: Mara nyingi ndoa za mastaa hazidumu. Je, umejipangaje na ndoa yako ili isivunjike? Jack: Kwanza ninamheshimu sana mume wangu na najiheshimu. Nimebadilika sana na ndoa yangu haiwezi kuvunjika milele. Funguka: Ni kitu gani unachokifurahia zaidi kwa mumeo? Jack: Nafurahia jinsi tunavyosikilizana na tunavyopendana. Funguka: Nashukuru kwa ushirikiano wako, nakutakia maisha mema ya ndoa. Jack: Asante sana, karibu tena.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...