Thursday, April 18, 2013

JOKATE ANASWA NA KIDUME!

Miss Temeke 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti‘ akiwa na mwanaume kimahaba imenaswa na kufi kishwa kwenye dawati la Amani.

Chanzo makini kimeitonya Centre Spread kuwa Jokate ameamua kujiweka kwa mwanaume huyo ambaye hakufahamika ili kulipa kisasi kwa aliyekuwa mpenzi wake,

Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alimuacha na kumchukua Peniel Mungilwa ‘Penny’. Baada ya kuinasa picha hiyo kwenye vyanzo vyake, paparazi wetu alimuendea hewani Jokate na kumshushia tuhuma hizo ambapo alileta hadithi njoo, utamu kolea: “Unajua kwa sasa nimeingia kwenye muziki na hivi karibuni nitatoa video yangu, unajua lazima kubadili fani, ndiyo maisha ya siku hizi na huyo mtu nimefanya naye video,” alisema Jokate kisha akakata simu.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...