Thursday, April 18, 2013

AHAHA WABUNGE HAWA MWE!OVER FILAM

FILAMU YA WABUNGE PART II ILIVYOANZA DOM

Unajua kinachoendelea kule mjengoni Dodoma katika Mkutano wa 13 wa Kikao cha Bunge la Bajeti la 2013/14? Kwa taarifa yako, ile filamu ya kauli za maudhi au tata katika bunge lililopita, inaendelea sehemu ya pili (part II), Amani lina kauli hizo. Katika vikao vya awali vya bunge hilo, tayari baadhi ya wabunge wameanza kutumia lugha za kuudhi na kuleta utata wakipigana vijembe kama ifuatavyo:

‘‘Mambo mengi nchi hii hayaendi kutokana na serikali pumbavu, hatuwezi kuwa na waziri wa elimu boya...” Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi

‘‘Kuna wabunge ambao wana mimba sizizotarajiwa bungeni...” Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde

‘‘Siongei na mbwa bali naongea na mwenye mbwa.” Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia

“UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma) kuna udini wa hali ya juu, wanafunzi wa dini tofauti hawalali chumba kimoja.” Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini

“Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.” Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa:

“Sikufurahishwa na kauli ya Lusinde kwamba tuna mimba sizizotarajiwa.” Anna Abdallah (Viti Maalum, (CCM)

“Kwa kuwa wanaume wengi wanabaka, kifunguliwe kituo wafundishwe kutongoza.” Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere

“Serikali iruhusu raia wa Tanzania walime bangi wapate fedha za kigeni.” Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally K

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...