Friday, April 19, 2013

DAVINA AJIFUNGUA

CHEREKO chereko zilitawala kufuatia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ kujifungua mtoto wa kiume kwa mumewe anayeishi naye sasa, Tabata, Dar.

Mama huyo wa watoto watatu sasa, alijifungua ‘baby boy’ huyo Jumapili iliyopita kwenye Hospitali ya Aga-Khan, jijini Dar na kusema anamshukuru Mungu kwa kwa hilo kama alivyokuwa akimwomba.

“Namshukuru sana Mungu nimejifungua salama, nilimwomba iwe hivyo. Kwa sasa namwomba Mola amjalie afya njema na maisha marefu mwanangu ili ikiwezekana naye aje kuwa mwigizaji kama mimi,” alisema Davina

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...