Wednesday, April 17, 2013

BI KIDUDE..

AMESHAZUSHIWA KIFO MARA KADHAA... Usiku wa kuamkia October 26, 2011 ujumbe ulisambazwa kwenye mitandao ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii, Facebook na Twitter kuwa Bi Kidude amefariki dunia! Moja ya SMS hiyo ilisomeka: Qaallu Inna Lillahi Wainna Ilaihi Raajiuni; BI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA! Habari ambazo zimekanushwa vikali na mwenyewe siku hiyo asubuhi. Kudhidirisha kweli hajafa, Bi. Kidude aliongea moja kwa moja na Radio One na kumwambia mtangazaji aliyetaka kujua ukweli wa habari hizo kwa kumjibu: "Maiti haiongei, mimi ndiye Bi Kidude, mzimaaa!" HII NI TABIA AMBAYO INAKUWA KWA KAZI YA KUZUSHIA WATU VIFO KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU NA KIJAMII

TUJIKUMBUSHE MATUKIO YA NYUMA:

MAISHA ALIYOISHI BI KIDUDE ENZI ZA UHAI WAKE

Maskini Bi Kidude! Ndiyo kauli pekee inayoweza kukuponyoka kinywani ukimtembelea Mwanamuziki mkongwe wa Taarab Bongo, Fatuma Binti Baraka ‘Bi Kidude’, Risasi Mchanganyiko limemshuhudia.

Maisha ya mkongwe huyo aliyeanza muziki mwaka 1920 akiwa na miaka 13, yanasikitisha (hohehahe) kutokana na kutokuwa na hadhi ya jina lake linalotambulika ndani na nje ya Bongo.

The 5 Star Paper, Risasi Mchanganyiko, mwishoni mwa wiki iliyopita lilitia maguu nyumbani kwake maeneo ya Raha Leo, Zanzibar na kushuhudia maisha magumu anayoishi staa huyo ambaye kwa sasa anakadiriwa kuwa na miaka 104.

Kwa mujibu wa Bi Kidude aliyezaliwa maeneo ya Mferejimaringo, Zanzibar, nyumba anayoishi imezeeka na haijamalizika kujengwa na hata kupakwa rangi kiasi ambacho mvua ikinyesha lazima alowe kama hataweza kukimbilia upande mwingine kutokana na kukosa kipato cha kuikamilisha.

Katika mahojiano yake na mwandishi wetu, staa huyo alifanya kazi ya kujitolea ya muziki kwa zaidi ya miaka 90 alisema, hakuna mtu asiyejua maisha magumu anayoishi kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anamfahamu vilivyo hivyo hana haja ya kujieleza zaidi kwa kuwa kila kitu kinaonekana kwa macho yasiyohitaji miwani.

Mkongwe huyo ambaye ni nembo halisi ya utamaduni wa Mtanzania alisema: “Siwezi kusema chochote juu ya maisha yangu mabaya kwani nitawaliza watu.

“Mtu yeyote ayatazame maisha yangu aone anachoweza kunifanyia kwani niliweza kuitangaza Jamhuri (Tanzania) vyema kwa maana hakuna nchi ambayo sijawahi kuitembelea kwa ajili ya kueneza utamaduni wetu.”

************************************************

BAADHI YA SHOW ALIZOWAHI KUFANYA JIJINI DAR ES SALAAM. HII ILIKUWA June 30, 2012

Hii ilikuwa usiku wa june 30 2011 katika ukumbi wa Equator uliopo Mtoni kwa Azizi Ally ambapo kulifanyika onyesho la taarab, wanamuziki mbalimbali wa taarabu waliudhuria akiwemo mwanamuziki mwalikwa toka Zanzibar Bi Kidude.

Baadhi ya bendi ambazo ziliudhuria onyesho hilo ni Five Star, TOT, East Africa Melod na Mashauzi classic

INNA LILAHI WAINNA

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...