Tuesday, February 5, 2013

ASKARI POLISI ATELEKEZA MTOTO ITUONI

ASKARI moja aliyekuwa zamu katika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Wilaya  ya Temeke jijini Dar es Salaam ambaye jina lake halikupatikana mara moja alipigwa na butwaa baada ya kutelekezewa mtoto (pichani) na raia mmoja Januari 26, mwaka huu.
Vyanzo vyetu vya habari vilidai kwamba siku hiyo mwanaume mmoja alifika kituoni hapo akiwa na mwanaye wa kiume mwenye umri wa miezi minne na aliwaeleza askari kwamba mkewe amemtelekezea mtoto huyo kisha kwenda  kusikojulikana.
Taarifa zaidi zilieleza kwamba
 baada ya baba huyo kufika ‘kaunta’ na kumweleza polisi aliyekuwa zamu kwamba hana pa kumpeleka mtoto huyo, aliwaomba wabaki naye kituoni hapo hadi mkewe atakapopatikana.
Habari hizo zilieleza kwamba polisi huyo alimweleza baba wa mtoto kwamba ampeleke kwa ndugu zake ili wamlee, ambapo
alikubali na kuamua kumfunga mtoto mgongoni lakini askari alipotoka kidogo akapata nafasi ya kumtelekeza  mwanaye juu ya meza pale kituoni na kutoweka.
Habari zinasema askari  aliporudi alimkuta mtoto akitabasamu akiwa juu ya meza lakini baba yake hakuonekana  kwa muda mrefu, ndipo walipoamua kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wazazi wake wanatafutwa.
Mwandishi wa habari hii alipofika Muhimbili, Afisa Ustawi wa Jamii Jengo la Watoto, Virginia Mwabena alikiri kuwepo kwa mtoto huyo hospitalini hapo.
‘‘Tuliletewa mtoto huyo na askari PC Bilikuza mwenye namba 5862 wa Kituo cha Polisi Chang’ombe akidai mtoto alitelekezwa na baba yake kituoni,” alisema afisa huyo.
Hata hivyo, wananchi waliokuwepo hospitalini hapo walilaani kitendo hicho cha wazazi kumtelekeza mtoto huyo asiye na hatia ambaye bado anahitaji malezi ya baba na mama yake.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...