Sunday, September 9, 2012

Zambia yajikongoja Kombe la Afrika


Timu ya Zambia
Timu ya Zambia
Zambia 1-0 Uganda
Zambia ilijipatia ushindi mwembamba dhidi ya Uganda wa goli moja kwa sifuri lililofungwa na mshambuliaji Christopher Katongo katika kipindi cha kwanza.
Goli hilo la upande wa Zambia lilikuja katika dakika ya 20 kwa ushirikiano mzuri wa Davies Nkausu.
Uganda hawakuonyesha makali na huenda wakajisikia unafuu baada ya kuondoka uwanjani wakiwa wamebebeshwa goli moja tu na Wazambia.
Uganda hawajawahi kupoteza mechi wakiwa nyumbani toka mwaka 2004, ingawaje safari bado inaendelea.
Pia katika mechi nyingine ilikuwa kama ifuatayo.
Jamhuri ya Kati(CAR) 1-0 Burkina Faso
Burkina Faso itabidi wachechemee katika raundi yao ya mwisho ya kufuzu kuingia mashindano ya Kombe la Afrika 2013 baada ya kufungwa goli moja na Jamhuri ya Afrika ya Kati(CAR) mjini Bangui siku ya Jumamosi.
Watajaribu kuthibitisha uwezo wao katika hatua nyingine mjini Ouagadougou mwezi ujao.
Kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliowaacha mdomo wazi mabingwa wa zamani wa Afrika Misri katika raundi za awali, matokeo haya yanawaweka katika nafasi nzuri kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa.
Gabon 1-1 Togo
Goli la kusawazisha kutoka kwa Emmanuel Adebayor aliyerejea timu ya Togo inaipa Togo nafasi nzuri katika mashindano haya baada ya kizaazaa cha mjini Libreville.
Ilikuwa ni Gabon walioleta muafaka baada ya mshambuliaji mkongwe Daniel Cousin kuipatia timu yake matumaini katika dakika 15 zilizokuwa zimesalia.
Lakini Adebayor, aliyerejea baada ya kutowekea mafichoni, alijibu mapigo na kuiweka Togo kuchungulia nafasi nyingine mjini Lome mwezi ujao.
Ghana 2-0 Malawi
Ghana imeiadhibu Malawi magoli mawili kwa bila ikiiacha Malawi kuwa na kibarua kigumu katika mapambano ya mbele.
Christian Atsu aliipatia Ghana mwanzo mzuri hususani katika dakika nane za kwanza.
Malawi ilijikuta ikijilazimisha kuzuia machozi baada ya James Sangala kutolewa nje wakati wa mchezo huo, na sasa wanakibarua kigumu kujibu iwapo wataingia fainali za mashindano haya ya Kombe la Afrika kwa mara ya tatu tu katika historia yao.
Sierra Leone 2-2 Tunisia
Siera Leone na Tunisia zimetoka sare ya mabao mawili kwa mawili huku matumaini ya Siera Leone kuingia fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa tangu mwaka 1996 yakiwa mashakani.
Alhassan Kamara aliongoza kwa kile alichodhania lingekuwa goli la ushindi dhidi ya Tunisia huku zikiwa zimesalia dakika tano tu mchezo kumalizika, lakini Youssef M'sakni akazawazisha katika dakika mbili baadaye.
Ivory Coast 4-2 Senegal
Ivory Coast waliibuka kidedea baada ya kuichapa Senegal magoli manne kwa mawili.
Dame N'Doye alianza kwa kuingiza goli la kwanza kwa Senegal, kabla ya Salomon Kalou kujibu mapigo.
Papiss Cisse aliipatia Senegal tabasamu baada kuongeza goli la pili kabla ya Ivory Coast kujibu mashambulizi kwa magoli kutoka kwa Gervinho, Didier Drogba na Max Gradel.
Goli jingine kutoka kwa Drogba lilikataliwa baada ya kuushika mpira kwa mkono.
Cape Verde 2-0 Cameroon
Cameroon ilijikuta ikiaibishwa hadharani baada ya kuchomekwa magoli mawili na Cape Verde, ikiwa ni matokeo mazuri kabisa kuwahi kupata kwa timu ya Cape Verde dhidi ya mabingwa hao wa mara nne barani Afrika.
Goli kutoka kwa Ricardo na pia Djaniny yamewapa matumaini Cape Verde kuingia katika fainali za mashindano haya kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao.
Kukosekana kwa Samuel Eto'o, kunaonekana kuipa Cameroon wakati mgumu sana kupata magoli, na ukweli ni kwamba wanahitaji magoli ili kuweza kuepuka fedheha za kutimuliwa kutoka katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.
Mali 3-0 Botswana
Licha ya mgogoro wa kisiasa nchini mwao Mali waliweza kuichapa Botswana magoli matatu kwa sifuri siku ya Jumamosi, ikijiweka katika nafasi nzuri kuelekea Afrika Kusini mwaka ujao.
Cheick Diabate anayeishi Ufaransa aliiwezesha timu yake ya nyumbani kuongoza katika dakika 27 za mchezo wakati wa goli la penalti, ambapo Mahamadou Ndiaye aliongeza la pili baadaye katika dakika ya sitini.
Naye Modibo Maiga hakuwa na huruma dhidi ya Botswana baada ya kushindilia goli la tatu lililoiacha Botswana ikitafuta mahali pa kujificha.
Ushindi huu wa magoli matatu unaipa Mali ujasiri wa kusonga mbele katika hatua ijayo mjini Gaberone pasipo kuwa na wasiwasi mkubwa sana.
Sudan 5-3 Ethiopia
Ilikuwa ni siku ya kuonyeshana ubabe wa nani zaidi katika kufungana magoli, wakati Sudan ilipoifunga Ethiopia magoli matano huku Ethiopia ikijibu kwa magoli matatu.
Ilichukua muda wa dakika saba tu kwa goli la kwanza kuchomekwa kutoka kwake Mudather El Tayeb Karika.
Hii ilileta hasira ya kuonyeshana nani ni mbabe zaidi katika mechi hiyo.
Katika ndani ya dakika mbili Momhmad Bisha aliipatia Sudan goli na Musab Umar kuimarsha zaidi katika dakika ya 36.
Baada ya mapumziko Ethiopia ilianza kuishambulia Sudan kwa magoli kutoka kwa Kebede na Tesfaye Alebachew yaliyoziweka timu hizo mbili katika usawa wa magoli matatu kwa matatu kabla ya mashambulizi mengine mawili kutoka kwake Muhannad El Tahir wa Sudan yaliyoiacha Ethiopia ikinyoosha mikono juu kukubali mvua hiyo ya magoli matano.
Liberia 2-2 Nigeria
Liberia ilitoka sare na Nigeria ya mabao mawili kwa mawili katika uwanja wa Samuel Doe Stadium mjini Monrovia
Omega Roberts aliipatia timu yake ya Liberia goli la kwanza katika dakika ya nane.
Lakini Nosa Igiebor alisawazisha kwa upande wa Nigeria dakika sita baadaye.
Ike Uche alifanikisha goli la pili kwa Nigeria kupitia penalti, wakati Vincent Enyeama alipoipatia pia timu yake goli la pili katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...