Thursday, September 20, 2012

WACHIMBA MGODI WAREJEA KAZINIWachimbaji wa Marikana

Wachimba migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurejea kazini katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana
Mgodi huo ulikuwa kitovu cha ghasia na mauaji ya wachimba migodi 44 waliozua ghasia wakati wakigoma kwa wiki sita kudai nyongeza ya mishahara .
Mapema wiki hii wachimba migodi waliafikia makubaliano ya asilimia 22 ya nyongeza ya mishahara ndipo wakakubali kurejea kazini.
Wamiliki wa mgodi wa Lonmin ambao ni wa tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya Platinum duniani, walielezea kupata hasara kubwa ya kifedha wakati mgodi huo ulipofungwa kufuatia mgomo wa wachimba migodi.
Jopo maalum limeundwa nchini humo kuchunguza vifo vya wachimba migodi waliouawa na polisi wakati wa migomo hiyo

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...