BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Thursday, September 13, 2012

Video: US consulate in Benghazi on fire, ambassador to Libya reported ki...


Naomba kukupa taarifa kwamba toka huu mwaka uanze, Nchi za Afrika zilizoshika namba nyingi na za juu kwenye habari kumi za Amplifaya mwaka huu ni Kenya, Nigeria na Libya ambako leo tena stori kamili kutoka kwenye hiyo nchi iliyowahi kutawaliwa na Muammar Gaddafi zinaamplfy kwamba Balozi wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi.
Nimechek na BBC, wameripoti kwamba Balozi J Christopher Stevens, ni miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kutokana na maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.
Idara ya mambo ya ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisa mmoja wa ubalozi huo ingawa bado haijataja jina lake ambapo maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo na kauli ya serikali ya Libya ni kwamba shambulio hilo ni kama kitendo cha uoga.
Huo ubalozi uliteketezwa na watu waliokua na bunduki waliolalamikia filamu moja iliyotengenezewa Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed.
Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na uhusiano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali walitumia mabomu ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya kuuteketeza, Kwa mara moja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...