Thursday, September 20, 2012

Mancini amkemea Kipa Joe Hart


Kocha wa Man City Roberto Mancini
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini amemuonya kipa wake Joe Hart dhidi ya kushutumu wachezaji wake, akisisitiza kuwa yeye pekee ndiye jaji.
Manchester City waliongoza mara mbili wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klbau bingwa barani ulaya dhidi ya Real Madrid, lakini walifungwa dakika za mwisho na mechi hiyo kumalizika huku Real Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Hart alisema haiwezekani kwa klabu yoyote ambayo inaongoza kwa mabao 2-1 huku ikiwa imesalia dakika tano za mechi na kasha ipoteze mechi hiyo. '' ni lazima sisi wenyewe tujilaumu'' aliongeza Hart.
Lakini Mancini amejibu kwa kusema, licha ya kukubalina na kipa wake, yeye anapaswa kutekeleza wajibu wake. ''mimi naweza kushutumu wachezaji wangu lakini sio Hart'' alisema Mancini.
Kabla ya mechi hiyo Manchester City ilikabiliwa na upinzani mkali kabla ya mchezaji wao wa ziada Edin Dzeko kufunga bao la kwanza kunako dakika ya 69.
Lakini Marcelo alizawazishia Real dakika saba kabla ya mechi kumalizika. Dakika mbili baadaya Aleksandar Kolarov aliifungia mabingwa hao wa England bao la la pili kupitia kwa mkwaju wa adhabu.
Karim Benzema na Cristiano Ronaldo walifunga bao moja kila mmoja dakika tatu za mwisho za mechi hiyo na kuisadia Real Madrid Kushinda kwa mabao 3-2.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...