Tuesday, September 18, 2012

MADAI: IRENE UWOYA SASA AIKIMBIA BONGO


Irene Pancras Uwoya.

ICON wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, anadaiwa kutimka Bongo huku taarifa zikidai yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kwenda kumwangukia mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’na nyingine zikisema yupo Msumbiji.
Kwa mujibu wa vyanzo makini viwili ambavyo vipo karibu na staa huyo, Uwoya hayuko Bongo, wikiendi iliyopita alikwenda kwa baba Krish kwani kwa sasa ana mawasiliano mazuri na mzazi mwenzie huyo.
Wakati chanzo kimoja kikieleza hayo, kingine kikarukia na kutonya kuwa Uwoya ambaye hivi karibuni alikuwa ‘lokesheni’ akirekodi filamu yake ya Apple, hakwenda kwa Ndiku bali yupo nchini Msumbiji.
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kuzungumza na Uwoya lakini hakupatikana, jambo lililosababisha mwanahabari wetu kufunga safari hadi nyumbani kwao Mbezi Jogoo jijini Dar na kumkuta msichana aliyejibu kuwa mama Krish hayupo na hajui aliko.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...