Friday, September 21, 2012

LINAH, AMINI WADAIWA KURUDIANA!STORI ambayo imetua kwenye meza ya dawati hili inadai kuwa, wale wanamuziki ambao ni mazao ya Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania ‘THT’, ambao walikuwa wapenzi kisha wakamwagana, Estelina Sanga ‘Linah’ na aliyekuwa mpenzi wake kitambo, Amini Mwinyimkuu sasa wamerudiana.
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa Linah kilidai kuwa, kurejea kwa penzi la wawili hao kumekuwa kwa siri sana na hakuna aliye tayari ivuje.
“Jamani, habari ndiyo hiyo, Linah na Amini, wamerudiana, kama vipi fuatilieni mtabaini hilo,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Katika kuweka mambo sawa, Ijumaa lilimtafuta Amini lakini simu yake haikuweza kupatikana mara moja. Linah alipopatikana hewani mahojiano na Ijumaa yalikuwa hivi:
Ijumaa: Vipi nasikia umerudiana na Amini nimeona picha ya kimahaba uko naye mtandaoni, ikoje hii?
Linah: Si umeiona picha…?
Ijumaa: Ndiyo…  kwani mmerudiana?
Linah: Ndiyo.
Ijumaa: Oke, lakini mbona hujaniambia siku zote hizo?
Linah: Nakutania…ni rafiki tu!
Ijumaa: Wewe muongo, kumbe ndiyo maana umemfagilia sana kwenye wimbo wako mpya eeh?
Linah:Kimyaaa..!
Hata hivyo, tunaendelea kuwawinda, tukiwanasa tutawaanika laivu.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...