Friday, September 14, 2012

KILICHOIKUTA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


Marehemu Daudi Mwangosi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.
Imekua ngumu kuwapata wahusika lakini millardayo.com inaendelea kuwatafuta ili kujua mazingira ya wizi na kama kuna ushahidi wowote uliopotea pamoja na mambo mengine,

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...