Tuesday, September 11, 2012

DK AULIWA KWA HAWARA


IGP, Said Mwema.
-AKUTWA PORINI AKIWA AMEOZA
Stori: Haruni Sanchawa, aliyekuwa Serengeti.
DAKTARI mstaafu, Thomas Mazela Tegero (66), anadaiwa kuuawa kwa hawara yake aliyetajwa kwa jina la Mkami Sendi, mkazi wa Kijiji cha Buchanchari wilayani Serengeti mkoani Mara kisha mwili wake kutelekezwa katika Pori la Magange lililopo kijijini hapo.
Daktari huyo mstaafu alifikwa na mauti Mei 16, 2012 na mwili wake kuokotwa Mei 22, katika pori hilo na kukutwa ukiwa umeshaanza kuharibika, huku ukiwa na majeraha sehemu za kichwani yaliyoonesha kuwa alipigwa na kitu chenye ncha kali kabla ya kuuawa.
Akizungumza na Uwazi, mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Thomas alisema baba yao kabla hajafikwa na mauti, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama huyo ambao ulianza kabla hajastaafu.
Godfrey aliendelea kueleza kuwa baba yao alistaafu mwaka jana na kulipwa mafao yake ya awamu ya kwanza.
Aidha, mtoto huyo wa marehemu aliendelea kueleza kuwa katika fedha hizo, baba yake alimkopesha mtoto mkubwa wa Mkami, Nyabite Sendi  kiasi cha shilingi milioni 12 kwa makubaliano ya kurejesha siku za baadaye.
“Ukoo wetu unaamini kuwa baba aliuawa na ndugu wa mwanamke huyo ili kupoteza ushahidi wa fedha alizokuwa anadaiwa Nyabite kwani hakuwa na uwezo wa kuzirejesha,” alisema Godfrey.
Aliongeza kusema kuwa baada ya baba yao huyo kuokotwa akiwa amekufa, nyaraka zake muhimu kama kadi benki ya NMB pamoja na kitabu chake cha kumbukumbu navyo vilipotea.
“Cha ajabu zaidi, kati ya siku hizo ambazo maiti ya baba iliokotwa, kuna mtu alienda benki kutoa kiwango kikubwa cha fedha akitumia kadi ya baba iliyopotea.
“Mpaka sasa kuna kiasi cha shilingi milioni mbili tu benki, fedha nyingine zote zimeshachukuliwa na wajanja,” alisema Godfrey
Baada ya tukio hilo, ndugu za merehemu walienda kuripoti polisi na kufungua jalada lenye namba BOR/RB/76/2012.
Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mara, Abslom Mwakyoma, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alithibitisha na kueleza kuwa upelelezi unaendelea kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...