Thursday, September 13, 2012

BANZA STONE: KARIBU NAKUFA


Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Stori: Gladness Mallya
MWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka kuwa amekata tamaa ya kuishi kwa vile ameota ndoto kuwa mwisho wake wa kuishi duniani umekaribia.
Akichezesha taya na paparazi wetu Jumatatu ya wiki hii jijini Dar, Banza alisema hivi karibuni aliota ndoto  anakufa na alioneshwa jinsi kifo chake kitakavyokuwa, ataugua ghafla na kufariki dunia.
Staa huyo wa muziki Bongo, alisema kufuatia ‘maono’ hayo, ameanza kutunga nyimbo ambazo zitazungumzia historia ya maisha yake.
“Ni kweli naona mwisho wangu umekaribia, nimeoneshwa ndotoni, inawezekana ni mpango wa Mungu ili nitengeneze maisha, nimeshaanza kuandaa albamu itakayohusu historia ya maisha yangu,” alisema Banza.
Banza aliendelea kutiririka kuwa, ndani ya moyo wake ana siri nzito ambayo ataitoa kwenye moja ya nyimbo zake lakini ni ya kusikitisha na ya kuhuzunisha.
Hata hivyo, alizidi kusema kwa masikitiko kuwa, baada ya ndoto hiyo hana raha ya kuishi tena na hajui yupo katika ulimwengu gani kwani anafikiria maisha ya ulimwengu mwingine atakaoelekea.
“Yaani mawazo yangu hayapo hapa, sijui niko dunia gani, nimekata tamaa, ninauona mwisho wa maisha yangu upo karibu lakini siogopi, natamani kufa kwa sababu ni lazima nitakufa hata nikiishi miaka mingapi,” alisema Banza.
Mwaka jana, staa huyo aliugua kwa muda na kulazwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na habari za mara kwa mara zilikuwa zikizusha kuwa amefariki dunia.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...