Tuesday, September 18, 2012

ALIYOYAZUNGUMZA MWIMBAJI PIPI KUHUSU NDOA YAKE YA KIMILA NA HUYU MTOTO WAKE.


Kingstone.
Tayari mwimbaji Pipi ameshaiandika kwenye kitabu chake cha kumbukumbu kwamba september 14 2012 ndio furaha nyingine ya maisha yake ilitimia baada ya kujifungua mtoto wa kiume ambae ni mtoto wake wa kwanza.
Mtoto anaitwa Kingstone jina lililochaguliwa na baba wa mtoto na linamaana nyingi ikiwemo Ufalme.
Pipi mwenye umri wa miaka 20 sasa hivi amesema hakutegemea kupata mtoto kwenye umri huo ila mume wake amechochea yeye kupata ujasiri na ameweza.
Pipi akiwa na Nikki wa Pili.
Kuhusu kupata lawama za yeye kujifungua akiwa na umri mdogo, namnukuu Pipi akisema “sijapata lawama zozote, familia yangu imefurahi, mama yangu amefurahi kwa sababu sijapata mtoto tu, kila kitu nafanya kihalali kwa sababu nina mume ambae kimila nimeshafunga nae ndoa lakini kanisani bado kwa sababu nilikua na ujauzito, mimi Mngoni lakini mume wangu anatokea Mtwara ni mmakonde”
Pipi Doreen ni staa wa single kadhaa za bongofleva ikiwemo first time, njia panda aliyoshirikishwa na Barnaba, pia kiujamaa ya Nikki wa Pili.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...