Friday, August 17, 2012

NDOA YA UWOYA YASUKWA UPYA,VIKAO VYAFANYIKAIrene Uwoya na mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’.

NDOA ya staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ina dalili za kurejea kwenye hali ya amani baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa, kuna vikao vinafanyika kwa lengo la kuihuisha.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake ambacho ni mmoja kati ya marafiki wa Irene kililitonya Ijumaa kuwa, yeye na watu wengine wa karibu wa msanii huyo wamedhamiria kuwarudisha wawili hao kwenye furaha kwani wanaamini bado wanapendana.
“Tunachokifanya sasa tunakutana mara kwa mara kuangalia kama tunaweza kutumia mbinu gani kuhakikisha ndoa ya Uwoya na Ndikumana inatengemaa. Kwa kifupi tunaisuka upya,” alidai sosi huyo na kuongeza:
“Unajua kwa watu unaowapenda huwezi kufurahi kuwaona wakiwa mbali, sisi tunaamini tutafanikiwa katika hili, tunajua Irene anampenda Ndiku na Ndiku anampenda Irene ‘so’ ni lazima kieleweke.
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Ijumaa lilimtafuta Irene ili kujua kama anajua lolote kuhusiana na vikao hivyo lakini hakuweza kupatikana.
Hata hivyo, Ndikumana aliwahi kuongea na moja ya magazeti ya Global Publishers na kusema kuwa hajavunja ndoa na Irene hivyo inaaminika siku yoyote mambo yatakuwa freshi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...