Friday, August 17, 2012

MASTAA WA MAKALIO YA KICHINA KIMENUKA


Na Hamida Hassan
MASTAA wa Bongo ambao wamekuwa na tamaa ya kusaka makalio ya Kichina kwa kutumia dawa mbalimbali, huenda sasa wakaachana na mpango huo baada ya kusoma habari hii ya mwanadada April Brown(Pichani), raia wa Marekani ambaye yamemkuta makubwa.
April ambaye alikuwa mwanamitindo, kutokana na tamaa yake ya kuwa na makalio makubwa, amejikuta akikatwa miguu na mikono baada ya kuchoma sindano zenye dawa za kumuwezesha kuwa na umbile hilo.
Akizungumza kwa masikitio na mtandao mmoja wa habari za kijamii, mrembo huyo alisema: “Ni tukio lililoyateteresha maisha yangu. Nilikuwa na umbile la kawaida tu lakini nikaingiwa na tamaa na kusaka makalio makubwa.
“Wapo walionishauri nitumie vidonge lakini baadaye nikaambiwa naweza kupata shepu hiyo kwa kuchoma sindano.
“Nilichoma sindano hizo kwenye zahanati bubu na mwanzoni niliona mabadiliko kwa kuongezeka lakini baadaye nikaanza kujisikia hali ya tofauti, nilipokwenda hospitali wakaniambia nimepata infections (maambukizi).
“Kadiri siku zilivyozidi kwenda, hali yangu nayo ilizidi kuwa mbaya na nilivyokwenda kwa daktari aliniambia kwa maambukizi niliyopata kutokana na kuchomwa sindano yenye silkoni inayotumika viwandani, ilikuwa lazima nikatwe miguu na mikono.
“Sikuwa na jinsi, ilibidi nikubaliane na ushauri wao na ndipo nilipopata kilema hiki,” anasema April ambaye sasa anaendesha kampeni ya kuwaelimisha wanawake wenzake juu ya madhara ya kutumia madawa ya kuongeza makalio.
Aidha, wakati kikiwa ‘kimenuka’ kwa April, Bongo kuna baadhi ya mastaa ambao wanadaiwa kutumia dawa za Kichina kwa lengo la kuongeza makalio na matiti yao.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umebaini kuwa, baadhi ya mastaa wamekuwa wakitamani kuwa na maumbile mazuri kama waliyonayo Wema Sepetu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ Agnes Gerald ‘Masogange’, Skaina Ally na wengineo.
Wakiongea na Ijumaa kwa nyakati tofauti, mastaa hao waliofungashia waliwatadharisha wenzao kutotumia dawa za Kichina kusaka makalio makubwa kwani yao ni orijino.
“Watu wasitafute kalio kama langu kwa kutumia Mchina, mimi nimepewa na Mungu hivyo kama wao hawajapewa basi wajikubali walivyo,” alisema Aunty Lulu.
Naye Agnes alisema: “Jamani madhara ya kutumia dawa za Kichina kuongeza maumbile zina madhara, tusipojiangalia tutajikuta tunajuta.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...