Friday, August 17, 2012

MKULIMA CHINA AJITENGENEZEA MIKONO YA BANDIA BAADA YA AJALI


Mkulima Sun Jifa akiwa katika shughuli zake akitumia mikono aliyojitengenezea.
MKULIMA mmoja nchini China aitwae, Sun Jifa ambaye mikono yake ilikatika kwenye mlipuko, ameamua kujitengenezea mikono yake ya bandia baada ya kuona gharama kubwa za huduma hiyo hospitali.
Sun (51) alipoteza mikono yake miwili baada ya kulipukiwa na milipuko aliyokuwa akiandaa kwa ajili ya uvuvi, lakini alishindwa kumudu mikono ya bandia aliyokuwa ameshauriwa na wataalamu hospitalini, hivyo kuwa na wazo la kutengeneza mikono yake mwenyewe.
Sun alitumia miaka minane akitengeneza mfano wa mikono aliyokuwa akihitaji ambayo inafanya kazi kwa kutumia mkusanyiko wa waya na mikanda inayomwezesha kunyanyua vitu.
Sun anasema “Nilipona lakini sikuwa na mikono na nisingeweza kugharamia mikono ya bandia hospitalini - hivyo niliamua kutengeneza mikono yangu mwenyewe.
Naimudu mikono yangu kwa kutumia viwiko  na naweza kufanya kazi, na kuendesha shughuli zangu zote kama mtu yeyote mwenye mikono halisi.
“Tatizo linalonikumba ni kuwa vyuma vya mikono hii ni vizito vinachosha, na vinaleta joto na baridi wakati wa majira ya joto au baridi.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...