Friday, August 17, 2012

HATIMAYE ALIYEKUTWA KACHOMWA NDANI YA GARI AZIKWA


Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Rehema.
Kaburi la marehemu Rehema Nungu.
MWANAMKE aliyeteketezwa ndani ya gari lenye usajili namba T883 BLA aina ya Toyota Corolla katika msitu wa Mabwepande, majivu ya mwili wake yalizikwa Agosti 15 mwaka huu katika makaburi ya Kondo, Tegeta Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Rehema Nungu aliteketezwa akiwa ndani ya gari na watu wasiofahamika.
Akitoa wasifu wa marehemu Rehema, katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa mumewe, Simon Sakilu, shemeji wa marehemu Vicent Lissu alisema mwenye taarifa zaidi za kifo hicho azipeleke jeshi la polisi mkoa wa Pwani. Alitoa kauli hiyo kutokana na kifo cha Rehema kugubikwa  na utata mzito na mkanganyiko wa hali ya juu na kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kupatikana kwa taarifa sahihi juu ya sakata hilo.
Lissu alisema siku ya mwisho marehemu alipatwa na msongo wa mawazo na alikuwa hazungumzi na mtu yeyote kwani ilifikia hatua ya kuzima simu yake ya mkononi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...