Tuesday, August 7, 2012

MKE WA SLAA ATEGEWA FUMANIZI


Dk. Wilbroad Slaa.
Mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi.
Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
KUNA taarifa kwamba mke wa Dk. Wilbroad Slaa, Josephine Mushumbusi ametengenezewa mtego ili afumaniwe na mume wa mtu.
Vyanzo vyetu vya habari vimesema kuwa mpango huo wa fumanizi umeandaliwa na chama kimoja cha siasa (jina tunalihifadhi) ili kumharibia Josephine na mumewe ambaye ni katibu mkuu wa Chadema katika medani ya siasa.
Mtoa habari wetu alibainisha kuwa maandalizi ya mpango huo yanafanyika Dodoma ambako kumekuwa na mikutano kadhaa ya wahusika ambapo mikakati inapangwa ya jinsi ya kumfumania na mume wa mtu ambaye tayari ameandaliwa na kuahidiwa kitita kikubwa cha fedha.
Habari zinasema kundi hilo limetengewa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya operesheni hiyo maalum inayoongozwa na kada wa chama kimoja ambaye jina lake linaanzia na herufi M.
Imeelezwa kuwa mume wa mtu aliyepatikana ameanza kazi kwa kumtumia Josephine ujumbe wa kimapenzi katika simu huku akimuahidi kitita kikubwa cha fedha.
“Huu ni mkakati wa kisiasa nia ikiwa ni kuwamaliza Dk. Slaa na mkewe katika ulingo wa siasa kwani Josephine akinasa basi umaarufu wa mumewe utakuwa umekwisha. Lakini habari hii siyo siri tena na waliopanga mpango huu wana hali tete baada ya kujua kuwa njama zao zimegundulika,” alisema mtoa habari wetu.
Gazeti hili lilipopata taarifa hizi liliwasiliana kwa njia ya simu na Josephine na alipoulizwa kama anajua chochote kuhusu mpango huo alikiri kufahamu.
“Ni kweli mpango huo upo na nimekuwa nikipokea SMS nyingi za kimapenzi na nimemuonesha Dk Slaa,” amesema Josephine juzi Jumapili.
Hivi karibu wakili maarufu nchini, Mabere Marando aliwahi kulalamika akidai kuna mtambo wa mawasiliano ambao umeingizwa nchini kinyemela ambapo mtu unaweza kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwa kutumia kifaa hicho, hali ambayo imesababisha watu mbalimbali waliozungumza na gazeti hili kudai kuwa inawezekana ndiyo unaotumika kumsumbua Josephine.
Nalo jeshi la polisi nchini, lilipoulizwa na gazeti hili kuhusu madai hayo, limesema linaendesha uchunguzi wa madai ya Marando.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema baada ya madai hayo kutolewa, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna anayefanya kitendo hicho, hatua kali sana zitachukuliwa.
“Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii. Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike,” alisema Senso
.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...