Tuesday, August 7, 2012

HUYU NDIO MSANII WA BONGOFLEVA ALIETANGAZA KUSHIRIKI BIG BROTHER MWAKA UJAO.


Jaffarai.
Siku moja baada ya Msanii wa Kenya Prezzo kuzikosakosa USD laki tatu za ushindi wa Big Brother Africa, Msanii wa bongofleva Jaffarai ametangaza bila kificho kwamba na yeye mwakani atajitokeza kugombea kuingia Big Brother.
Exclusive na millardayo.com J amesema “nafikiria kitu kama hicho unajua kwa sababu nimeanza kufatilia Big brother miaka mingi sana na hii ya mwaka huu kidogo imenivutia kwa sababu watu wengi walikua wanaamini Prezzo angeshinda mimi pia ni mmoja wao, pia imefanya watu waamini kwamba kushinda BBA sio lazima uwe mapepe sana sometimes unaweza ukawa mtu flani cool ukashinda vilevile”
Jaffarai ambae ni mkazi wa Kijitonyama Dar es salaam ameongeza kwenye line nyingine kwamba “BBA ni nzuri kwa wasanii wa muziki hata movie kwa sababu unaonekana alafu nimegundua sio lazima kushinda hela kuna kushinda vitu vingi mtu kama Prezzo hajashinda hela lakini ameshinda vitu vingine tofauti kabisa, ameweza kujitangaza tofauti na mwanzo alafu atapata mikataba flaniflani, pia nafasi ya kwenda kwenye show ya Jay Z na inakua rahisi hata akitoa ngoma zake kusikika sehemu nyingine”
Unafikiria nini kuhusu uamuzi wa Jaffarai, una chochote cha kumshauri, kuna uwezekano wa yeye kufanya vizuri?

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...