BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Tuesday, August 7, 2012

Gharika yasababisha mafuriko Manila


Mafuriko Manila
Idadi kubwa ya watu wameripotiwa kufariki kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku nzima na kusababisha mafuriko katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila.
Mafuriko hayo ambayo yamesababisha athari kubwa katika baadhi ya maeneo, yamewalazimisha maelfu ya watu kutoroka makwao huku mashule, afisi za serikali na soko la hisa zikishindwa kuendelea na shughuli za siku kutokana na maji yanayoaminiwa kufikia kiunoni.
Familia moja ya watu wanane waliangamia baada ya maporomoko ya ardhi kuangusha nyumba nyingi kwenye mitaa duni mjini Quezon.
Mvua zaidi inatabiriwa kunyesha katika siku mbili zijazo.
Mji wa Manilla na maeneo mengine kaskazini mwa nchi hiyo zimekumbwa na hali mbaya ya anga tangu kutokea kimbunga cha Saola yapata wiki moja iliyopita.
Kufikia sasa takriban watu hamsini wamethibitishwa kufariki kufuatia gharika iliyotokea wiki mbili zilizopita.
Watu wakimbilia usalama wao
Mafuruko makubwa yanatabiriwa kutokea katika mji mkuu na viunga vyake pamoja na mikoa mingine kulingana na taarifa ya baraza la utabiri na udhibiti wa majanga nchini humo.
Kinachowatia wasiwasi watu wengi nchini humo ni kuwa mvua imekuwa ikinyesha kwa masaa 24 na kwamba mvua kama hii ndiyo iliyosababisha mafuriko baada ya kimbunga Ketsana mwaka 2009.
Wakati huu serikali inasema imejiandaa vyema kukabiliana na hali hiyo na hadi sasa imeweza kuwahamisha maelfu ya watu kutoka maeno yenye mafuriko.
Manusura wa mafuriko Ufilipino
Lakini watu wengi hawataki kabisa kuhama hasa ikiwa hawawezi kuchukua mali zao,wengi wameonekana wakirejea kwenye maji kwenda kwa nyumba kuweza kunusuru mali zao.
Rais Benigno Aquino tayari amekutana na maafisa wa ulinzi kujadili mipango ya usalama na kwamba kila mtu ambaye ana jukumu la ulinzi tayari wamejiandaa.
Maafisa wa serikali wamelazimika kutangazia watu kuchukua hatua za dharura ili kujilinda kutokana na hatari zozote hasa baada ya watu wanne kuripotiwa kufa maji katika mkoa mwingine ingawa taarifa hizi bado hazijathibitishwa.
Wakuu wa utabiri wa hali ya hewa, wameonya kuwa mafuriko huenda yakawa makubwa zaidi hasa baada ya bwawa kubwa la "La Mesa" kufurika.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...