Saturday, August 11, 2012

Flora Mvungi "Sikumfukuza Shilole Nyumbani Kwangu"


NGOMA iliyofanya vizuri ya msanii Zena Muhamedi ‘Shilole’, ‘Nyumba za Kupanga Lawama’, inadaiwa kuwa ilikuwa inamlenga rafiki yake wa karibu, Frola Mvungi, kwani ndiye aliyempokea na kumkaribisha kwake pindi alipotoka mkoani lakini walikuja kutengana baada ya Mvungi kuanza kumtupia maneno machafu kuwa akapange kwake.

Mvungi baada ya kusikia maneno kuwa ngoma hiyo ametungiwa maalumu kwa ajili yake, aliongea na DarTalk ili kueleza nini kilichosababisha hadi wimbo huo uwe kijembe kwake, ambapo alidai kuwa ni kweli alimpokea Shilole, lakini hakumfukuza kama anavyodai mwenyewe.

Frola alidai kuwa haoni sababu ya yenye kutungiwa wimbo huo kwani alitumia busara ya kumchukua Shilole pindi alipotua jijini kwani alimsaidia kama rafiki lakini baada ya muda waliishi kama ndugu na hakumfukuza bali yeye ndiye aliamua kuondoka na kupanga kwake.

“Huo wimbo nimesikia watu wanazungumza lakini sioni kama alichokifanya ni kizuri kwani, mimi nilimsaidia hadi kulijua jiji la Dar, ingawa nashukuru kwani mungu ndiye atakayenilipa kwa mema niliyomfanyia,” alisema Mvungi.

Hata hivyo kauli ya muhusika wa wimbo, Shilole, “Nilitunga huu wimbo kwa sababu zangu kwa hapa dar nyumba za kupanga zina lawama sana hivyo kama Frola anaona wimbo wangu unamlenga yenye basi hizo ni fikra zake,” alidai.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...