Saturday, August 4, 2012

ALIYOZUNGUMZA TAMEKA RAYMOND KWA MARA YA KWANZA TOKA UTOKEEE MSIBA WA MWANAE NDIO HAYA.


Marehemu Kile na mama mzazi Tameka.
Zikiwa hata wiki mbili hazijaisha toka mke wa zamani wa mwimbaji Usher Raymond Tameka Raymond kumzika mwanae kipenzi Kile aliefariki dunia kwenye ajali iliyotokana na pikipiki zinazoendeshwa kwenye maji, Mama huyu wa watoto watano ametoa kauli ya kwanza toka msiba utokee.
Tameka ambae kwa kipindi kirefu amekua mahakamani kutokana na kesi ya kugawana watoto yeye na mumewe wa zamani Usher Raymond, amesema hii statement haijaandikwa na timu yake, msaidizi wake wala yeyote bali ni maneno ambayo ameyaandika kutoka moyoni mwake.
Ripoti yake inasema hivi “Kwa majonzi makubwa nimejikuta nikilazimika kujibu waraka wa mahakama unaonitaka nifike Mahakamani kwenye kesi ambayo sio mimi niliyeianzisha, sikumshitaki mtu yeyote kwenye hii kesi ya January 2011 japo niliridhika na maamuzi ya  ya kugawana majukumu kuwalea watoto”
“Kinachonisikitisha ni kulazimika kwenda Mahakamani katika kipindi ambacho naomboleza kifo cha mwanangu, hata hivyo sitozuia Mahakama kufanya kazi yake, nitaendelea na yale yote nitakayolazimika kuyafanya huku nikiwa na matumaini kuwa hali hii ngumu itanisaidia kupambana na hali nyingine ngumu zaidi ya majonzi ya mwanangu” – Tameka
Kwenye line ya mwisho, Tameka mwenye umri wa miaka 41 amesema “naisihi jamii yote kutoamini yale yote yanayosikika kwenye vyombo vya habari na pia jamii isiwe nyepesi ya kuhukumu, wanangu ndio ulimwengu wangu na nitapambana kufa na kupona kuwalinda na kuwa nao maisha yangu yote”
Hiyo ni taarifa kupitia mtandao wa Global Grind, Hallo Beautiful wameripoti kwamba Usher Raymond hakutoa ushirikiano wowote kipindi cha msiba na hakuwahi kuongea na Tameka wala familia yake, pia alikwenda kumzika Kile kwa sababu tu tayari anajulikana kwamba ni mtoto wake wa kufikia na vyombo vya habari na watu wengine walitegemea kuona angefanyaje kwenye maziko ya mtoto wa mke wake wa zamani.
HBL wameripoti zaidi kwamba taarifa zilizopo ni kwamba wakati wote wa msiba Usher alikua hapokei simu za Tameka wakati alipohitajika kutoa msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya Kile alipokua

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...