Kuna vitu vingi nilikua 
navisikia vinatokea kwenye uwanja wa Taifa Temeke tu lakini 
sikuvitarajia kama leo ningesikia vinatokea au vitatokea London.
Ukisikia mtu kaibiwa simu 
uwanja wa Taifa Temeke au ticket za bandia kuuzwa sio kitu kigeni, ni 
kitu ambacho hata mimi nimewahi kukutana nacho.
Sasa toka Olympic 2012 kuanza nimepata stori mbili ambazo kwa upanda mwingine zinashangaza na kufurahisha pia.
Baada ya juzi shirika la habari
 la Reuters kutangaza kwamba maafisa wa usalama wamethibitisha kwamba 
kutokana na hali ya kiusalama huenda watu elfu 67 wakaibiwa au kupoteza 
simu zo kwenye Olympic 2012 hasa simu za gharama.
Leo Sky News Break wameripoti 
kwamba tayari Polisi wamekamata watu 29 ambao wamekua wakiuza ticket 
bandia za kuingia kwenye michuano hiyo toka ianze ijumaa iliyopita 
july27 2012.
Unaweza kulike au kutweet hii post ili na wenzako waione.

No comments:
Post a Comment