WOLPER AFUNGUKA SKENDO YA KUNYANG'ANYWA GARI
 |
| Wolper |
TETESI
zimezagaa jijini Dar es Salaam kuwa staa wa sinema Bongo, Jacqueline
Wolper Masawe amenyang’anywa lile gari lake aina ya BMW X6, lenye namba
za usajili T 574 BXF na kwamba, sasa nyota huyo anatembelea gari lake la
zamani Toyota Noah, Amani limeshibishwa taarifa.
Chanzo cha kuenea
kwa tetesi hizo kilianzia kwenye mitandao ya kijamii, hasa blog na BBM
ambapo wadau waliandika kuwa Wolper alinyang’anywa gari hilo na mwanaume
aliyemnunulia.
Aidha, wadau wengine walikwenda mbele zaidi wakitaja
jina la Frank ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar kuwa
ndiye mmiliki wa gari hilo kwa sasa.
Baada ya kupata taarifa hizo,
Jumatatu wiki hii, saa saba mchana timu ya Amani iliingia mzigoni kusaka
ukweli wa taarifa hizo ambapo mtu wa kwanza kuzungumza naye alikuwa
Wolper mwenyewe ambaye alikiri kusikia taarifa hizo huku akikanusha kuwa
si za kweli.
 |
| Gari inayodaiwa wolper kunyanganywa |
“Na mimi nimesikia lakini si kweli jamani. Hivi mtu
anaweza kunyang’anywa nguo yake ya ndani au shati lake? Si itakuwa
kichekesho, gari ni mali yangu na hakuna mwenye uwezo wa kuja
kuninyang’anya kwani nalimiliki kihalali,” alisema Wolper.
Aidha,
staa huyo mwenye kuandamwa na matukio kwa siku za karibuni, alisema
amelifungia gari hilo nyumbani kwake, Mbezi Beach, Dar kwa sababu lina
matatizo kidogo.
Amani halikukubaliana na utetezi wake, likamtaka
Wolper kuongozana na mapaparazi wake ili kwenda Mbezi kuliona gari hilo
kama lipo kweli au kulifikisha ofisi za Global.
Wolper:
“Nisikuongopee kuwa naweza kuja nalo hapo ofisini wakati tatizo lake
nalifahamu mimi, nakuja kuwachukua twendeni nyumbani mkalione.”
 |
| wolper akionyesha kadi ya hiyo gari |
Saa 2:16 usiku, Wolper aliongozana na mapaparazi wetu hadi nyumbani kwake na kulikuta gari hilo likiwa ndani ya geti.Katika hali isiyokuwa ya kawaida, staa huyo alilionesha gari hilo huku akimwaga machozi na kusema:
“Watu
wananionea sana, wananichafua. Sijui lengo lao ni nini hasa? Kila
kukicha nasingiziwa jambo, mara Jack kafanya hivi, mara vile.
“Mbaya zaidi, hata waigizaji wenzangu wapo wanaonichukia, au kwa kuwa nimepata maendeleo kidogo? Walitaka niporomoke kimaisha?”
Licha ya kupata uhakika kuwa Wolper hajanyang’anywa gari hilo, pia alionesha kadi yake ya umiliki.
No comments:
Post a Comment