MCHEZASINEMA WA MAREKANI DEIDRE LORENZ, ATUA MJINI MOSHI NA SHAUKU KUBWA YA KUONA MLIMA KILIMANJARO KAMA KWELI UPO TANZANIA

Mcheza
sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari
kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Juni
24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio
wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika Jumapili ya
mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.
Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule,
Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu
mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu
ambayo yanaendana na hadhi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza
sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko
Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili
kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa
nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu
pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie
niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa
zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka
mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo
jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema
Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City
linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la
kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo
karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya
Uhuru Park.
Mji wa Moshi na viunga vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi
kutoka Marekani ambao wamekuja kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea
umaarufu mkubwa kwa kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances mwaka 1991 baada ya
kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania nchini Misri.
Mbio hizi zimejijengea umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo
nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na Wonders of the World Magazine lenye
wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye
hadhi ya kukimbiwa duniani wakati jarida la Forbes la Marekani lenye
wasomaji wengi duniani limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya
Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.
Mbio hizi hukimbiwa na watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda
mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro
Marathon zinajulikana kama 7 continental races zikiwa zinakimbiwa katika
mabara 7 ya dunia.
Ratiba ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea
kituo cha watoto yatima cha Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious
Blood. Lorenz atakaa na watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za
watoto zilizoandikwa na Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne ya
ishirini wa Marekani.
Siku ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC ambapo atakutana na
manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya
jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na
wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia kesho yake siku ya
jumapili tarehe 24 juni.
No comments:
Post a Comment