BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Thursday, June 28, 2012

UNA HABARI KWAMBA BEEF YA HAWA JAMAA IMEKWISHA?


Big Sean na Ludacris.
Kila ambae sikio na macho yake viko kwenye aina ya muziki wanaoufanya hao washkaji hapo juu ni lazima awe anafahamu kwamba walikua kwenye beef ndefu kidogo ambayo ilikua ni kulumbana baada ya Luda kumind Big Sean na Drake kudai kwamba amekopi flow yao.
Haukua mtiti mdogo manake Luda pia alifikia mpaka kurekodi single inaitwa Bada boom kama Diss kwa Drake na Big Sean ambao walimdis huku Drake akisema hawamkatazi mtu kuchukua flow yao lakini achukue na aitendee haki sio kuiharibu, akimaanisha Luda aliharibu.
Luda alipanic mpaka kusema yeye ni MC wa siku nyingi kwenye game, hakuna ambacho anaweza kufundishwa na hao vijana wapya, na ana stile nyingi za kurap kuliko rapper yeyote kwenye game, ana miaka 11 katika anachokifanya na bado mkwanja na bado anaendelea kucount wakati hao vijana wananyimbo chache tu.
Mpaka November mwaka jana Big Sean hakuwa na kiherehere sana kama Drake kwenye kujibu hiyo diss na mara nyingi alikua akijiepusha, nakumbuka Sean kwenye interview na Seattle’s KUBE 93 radio station alisema hataki ugomvi na Luda na wala hakufikiria kama bado Luda alikua anafikiria hiyo ishu kwa mwaka mzima, Luda ni Mkongwe na ni mmoja kati ya wakali anaowatambua.
MTV imesema Luda ametangaza kumaliza beef na Big Sean kwa kusema walikutana Australia kwenye show wakakaa kuyaongea na kuyamaliza, Sean nae on BET alisema wameyamaliza na Luda.
Ngoma imebaki kwa Drake time hii tuendelee kusikilizia….

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...