Ujerumani yafuzu kwa robo fainali
Lars Bender alifunga bao la ushindi la Ujerumani siku
ya Jumapili zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho, na
kuiwezesha nchi yake kuwa miongoni mwa nchi nane ambazo zitashiriki
katika michuano ya robo fainali.
Mechi nyingine ya kundi hilo la B ambayo
ilichezwa wakati mmoja, kati ya Ureno na Uholanzi, Ureno walifuzu kwa
ushindi kama huo wa magoli 2-1.
Bender,
mwenye umri wa miaka 23, na ambaye ni mchezaji wa Bayer Leverkusen ya
Ujerumani, aliizima ndoto ya Denmark ya mwaka 1992, walipowashinda
Wajerumani katika fainali.
Ujerumani iliweza kuongoza katika mechi hiyo
dakika ya 19 wakati Lukas Podolski alipofunga, lakini Michael
Krohn-Dehli aliweza kuisawazishia Denmark dakika sita baadaye na
kuipatia nchi yake matumaini ya kufika robo fainali.
Wachezaji wa Ujerumani hawakupendezwa na safari
kutoka kituo chao cha nyumbani cha Gdansk, Poland, hadi Ukraine, lakini
kutokana na ushindi wa Lviv, wameweza kufuzu kuingia robo fainali na
watafurahia kuicheza mji ambao wameezeka kambi yao.
Kabla ya mechi ya Jumapili, mara ya mwisho
Denmark ilipopambana na Ujerumani katika mashindano makubwa, ilikuwa ni
fainali ya 1992, wakati Yugoslavia ilipopigwa marufuku kucheza, na
hatimaye Denmark iliwashangaza wengi ilipoishinda Ujerumani katika
fainali.
Timu ya Ujerumani ya mwaka huu ndio timu yenye
vijana wenye umri mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huu, kwa jumla
wachezaji wengi wakiwa na umri wa miaka 25 na siku 107.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kukamilisha mechi za makundi kwa rekodi safi mno ya asilimia 100.
No comments:
Post a Comment