Rooney ni nyota ya England
Kufuatia adhabu ya UEFA Rooney alizikosa mechi mbili za kwanza za England
Wayne Rooney alikaribishwa kama
shujaa katika timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa
muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine
liliiwezesha timu yake kuwa kileleni katika kundi la D.
Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.
Rooney,
akiwa karibu sana na kipa wa Ukraine, Andriy Pyatov, aliweza kufunga
kwa kichwa, mpira uliokuja juujuu kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.
Licha ya England kuibuka washindi, Ukraine
walifanya juhudi kubwa na kupata nafasi nyingi zaidi za kusawazisha,
lakini yote hayo hayakufua dafu.
Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa
Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John
Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba
kweli mpira haukuvuka msitari.
Ushindi wa Sweden wa magoli 2-0 dhidi ya
Ufaransa ulihakikisha kwamba England wanafuzu kuingia robo fainali kama
timu iliyoongoza katika kundi D.
No comments:
Post a Comment